Kaimu Kamishna wa Madini, Mhandisi Ally Samaje akiwasilisha mada

kuhusu Sekta ya Madini – Tanzania kwa Waziri wa Nishati na Migodi 

wa Burundi, Mhe. Côme Manirakiza (wa kwanza kulia) na Ujumbe wake 

(Kulia kwake) waliofika Makao Makuu ya Wizara – Dar es Salaam, Agosti 

26, 2014 kujifunza namna Sekta za Nishati na Madini zinavyofanya kazi. 

Upande wa kushoto ni Wataalamu mbalimbali wa Wizara na Taasisi zilizo 

chini yake.

Mtaalamu kutoka Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC),

Wellington Hudson akitoa mada kuhusu Rasilimali za Gesi na Mafuta

kwa Waziri wa Nishati na Migodi wa Burundi, Mhe. Côme Manirakiza

(Wa kwanza Kulia) na Ujumbe wake. Ujumbe huo ulifika Makao Makuu

ya Wizara – Dar es Salaam, Agosti 26, 2014 kujifunza kuhusu Sekta za

Nishati na Madini zinavyofanya kazi. Wengine pichani ni Wataalamu wa

Wizara na Taasisi zilizo chini yake wakiongozwa na Kaimu Kamishna wa

Madini, Mhandisi Ally Samaje (wa kwanza kushoto).

 Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Jiolojia Tanzania (GST), Profesa Abdulkarim 

Mruma (aliyeinua mikono), akitoa ufafanuzi kuhusu GST kwa Waziri wa 

Nishati na Migodi wa Burundi, Mhe. Côme Manirakiza (Wa kwanza Kulia) 

na Ujumbe wake waliofika Makao Makuu ya Wizara - Dar es Salaam, 

Agosti 26 kujifunza namna Sekta za Nishati na Madini zinavyofanya kazi.
Mtendaji Mkuu wa Jiolojia na Migodi (Geology and Mines) wa Burundi,

Emmanuela Ngenzebihoro (mwenye kilemba) akiuliza swali kwa

Wataalamu wa Wizara ya Nishati na Madini – Tanzania (Walioketi

Kushoto), wakati wa ziara ya Waziri wa Nishati na Migodi wa Burundi,

Mhe. Côme Manirakiza (Wa kwanza Kulia) na Ujumbe wake Makao

Makuu ya Wizara - Dar es Salaam, Agosti 26, 2014. Waziri Manirakiza na

Ujumbe wake walifika wizarani kujifunza namna Sekta za Nishati na Madini

zinavyofanya kazi.


Waziri wa Nishati na Migodi wa Burundi Mhe. Côme Manirakiza (aliyeinua 

mkono), akiomba kupewa ufafanuzi kuhusu sekta ya madini hapa nchini, 

baada ya uwasilishwaji mada zilizohusu sekta za nishati na madini za 

Tanzania. Waziri Manirakiza na Ujumbe wake walitembelea Makao Makuu 

ya Wizara ya Nishati na Madini - Dar es Salaam, Agosti 26, 2014 kwa 

lengo la kujifunza namna sekta husika zinavyofanya kazi. Wengine pichani 

ni Wataalamu wa Wizara ya Nishati na Madini - Tanzania (kushoto) na 

Ujumbe ulioongozana na Waziri (Kulia).

Na Veronica Simba




Waziri wa Nishati na Migodi wa Burundi, Mhe. Côme Manirakiza na

Ujumbe wake wako katika ziara ya siku tano (24 – 28 Agosti, 2014)

hapa nchini kwa lengo la kujifunza namna Sekta za Nishati na Madini

zinavyofanya kazi.

Katika ziara yake, Waziri Manirakiza ametembelea Makao Makuu ya

Wizara ya Nishati na Madini – Dar es Salaam na kukutana na Wataalamu

mbalimbali wa Wizara na Taasisi zilizo chini yake wakiongozwa na Kaimu

Kamishna wa Madini, Mhandisi Ally Samaje.


Wakiwa Wizarani, Waziri na Ujumbe wake walipata fursa ya kusikiliza

mada zinazohusu Sekta za Nishati na Madini zilizowasilishwa na

Wataalamu wa Wizara.

Ujumbe huo pia umepata nafasi kutembelea Taasisi na Mashirika

mbalimbali yaliyo chini ya Wizara na yale yenye uhusiano na Wizara

ikiwemo Mpango wa Uwazi na Uwajibikaji katika Tasnia ya Uziduaji

Tanzania (Tanzania Extractive Industry Transparency Initiative – TEITI),

Mradi wa Usimamizi Endelevu wa Rasimali Madini (SMMRP) na Wakala

wa Ukaguzi wa Madini Tanzania (TMAA).