Mawaziri wa afya wa Afrika Magharibi wanakutana Ghana kutafita njia za kupambana na Ebola
Shirika la afya duniani WHO limeonya kuwa mlipuko wa ugonjwa wa Ebola huko Afrika magharibi huenda ukasambaa na kuwaambukiza zaidi ya watu 20,000 kabla haujadhibitiwa.
Kwa sasa idadi ya waliothibitishwa na kuorodheshwa kuambukizwa ni elfu 3 ingawaje inashukiwa kuna wengi wengine ambao hawajajulikana.Zaidi ya watu 1500 wamefariki kutokana na mlipuko wa sasa wa Ebola wengi wao wakiwa ni wa kutoka Liberia,Sierra Leone na Guinea.
Mkurugenzi wa WHO katika kanda hiyo - Dr Lious Sambo - ameeelezea jinsi wafanyikazi katika kliniki za wagonjwa wanavyo'ng'ang'ana wakijaribu kukabilianana na janga hilo la Ebola.
Wauguzi ni wachache ilihali wanapaswa kusaidia haraka inavyowezekana
Wagonjwa watano wa Ebola pia wamefariki Nigeria .
Mawaziri wa afya katika eneo hilo la Afrika magharibi wanakutana nchini GHana kujadili janga hilo.
Mkurugenzi wa MSF huko Liberia, Brice de la Vigne, ameiambia BBC vitanda zaidi ya elfu vinahitajika huko Liberia kwa minajili ya kuwatenga wagonjwa wa Ebola.
|
0 Comments