Kwa mujibu wa chanzo chetu makini cha habari ambacho kimeshuhudia sakata hilo mwanzo mwisho, ishu nzima ilianzia maeneo ya Makumbusho ambapo gari alilokuwa akilitumia Kibonde, liligonga kwa nyuma gari jingine na kisha kukimbia.
“Baada ya kugonga, Kibonde alirudi nyuma kisha kuanza kukimbia ambapo trafiki alitumia gari lililogongwa na Kibonde kumkimbiza,” kilimwaga data chanzo hicho.Chanzo hicho kilifafanua kuwa baada ya polisi kumkimbiza kwa saa kadhaa, walifanikiwa kumkamata maeneo ya Mwenge ambapo trafiki alipanda kwenye gari la Kibonde na kumuamuru arudi eneo la tukio lakini Kibonde hakuwa tayari kurudi ndipo alipoanza kukimbia tena, huku askari aliyemkamata akiwa ndani ya gari.“Inaonekana kulitokea kutoelewana kati ya askari na Kibonde ndipo askari huyo alipowasiliana na wenzie kwa njia ya radio call ili wambananishe na alipofika Ubungo kwenye mataa wakamtaiti na kumpeleka kituoni, Oysterbay,” kilihitimisha chanzo chetu.
Baada ya kupata maelezo hayo, kachero wa Ijumaa Wikienda alitia timu katika kituo cha Oysterbay ili kutaka kujua mustakabali mzima wa ishu hiyo ambapo alimshuhudia Kibonde akiwa amesimama nyuma ya nondo huku akiwa anaimba ‘nyimbo’ anazozijua mwenyewe.
Mtangazaji huyo amefunguliwa kesi iliyopewa RB namba OB/RB/13806/20014 KUGONGA NA LUGHA YA MATUSI.
0 Comments