Baadhi ya wafanyakazi Kampuni ya Kupakua na Kupakia Kontena Bandarini (TICTS) wakiwasili kwenye ufukwe wa bahari ya hindi maeneo Kata ya Kivukoni kwa ajili ya kushiriki zoezi la kusafisha fukwe hizo katika kuhitimisha kampeni usafi iliyokuwa ikiendeshwa na Kampuni ya Green Waste Pro Ltd mwishoni mwa juma.
Na Mwandishi wetu
KAMPENI kubwa ya kuhamasisha usafi iliyokuwa inaendeshwa kampuni ya Green Waste Pro Ltd katika kata tatu za katikati ya jiji imemalizika kwa ufanisi mkubwa kiasi cha kufanya eneo hilo kumeremeta tena.
Kampeni hiyo ambayo ilianza Septemba 6 mwaka huu ilifungwa kwa usafi katika kata ya Kivukoni ambapo kampuni ya TICS ilishiriki kufanya usafi katika fukwe za bahari.
Katika kampeni zilizoshirikishwa wadau mbalimbali wa mazingira na afya katika kuhamasisha usafi miongoni mwa wananchi pamoja na kufanya usafi viongozi walitumia nafasi hiyo kufunza watu umuhimu wa kushiriki katika kufanya usafi na kuwa wasafi.
Kata zilizohusika na kampeni hiyo ni kata ya Kisutu, Mchafukoge na Kivukoni.
Meneja Kitengo cha Makontena TICTS, Bw. Donald Talawa alisema usafi huo umelenga kuweka maeneo ya bandari kuwa masafi na japokuwa wao wapo Temeke waliona kuna kila sababu ya kushiriki usafi kwenye maeneo ya bahari ambayo wanafanyia kazi.
Naye Afisa Mtendaji wa Kata ya Kivukoni Bw. Renatus Ruhungu alisema kampeni hiyo ambayo imefanikiwa, ilikuwa inawakumbusha wananchi wajibu wa kushiriki katika kuweka maeneo safi .
Baadhi ya wafanyakazi wa Kampuni ya TICTS, kampuni ya usafi ya Green Waste Pro Ltd na watendaji wa halmashauri pamoja na viongozi wa kata ya Kivukoni wakichukua vitendea kazi tayari kuanza kusafisha fukwe za bahari ya hindi.
Alisema katika kampeni hiyo wamefanikiwa kushawishi wananchi kutambua kwamba usafi si kazi ya serikali pekee bali hata wao na kwamba eneo linapokuwa safi ni sifa ya wananchi na wahusika wengine.
Aliwataka wananchi waguswe kuwa suala la usafi si la serikali bali la kila mmoja kutokana na ukweli kuwa wanapougua kutokana na mazingira kuwa machafu ni tatizo binafsi zaidi japokuwa serikali itawajibika kusaidia tiba.
Alisema pia kwamba ushiriki wa TICTS katika kampeni hizo siku za mwisho kunadhihirisha kwamba suala la usafi halina mipaka kwani kila mmoja linamgusa kwa namna moja au nyingine hata kama hakai eneo lile.
Eneo ambalo limefanyiwa usafi ni lile ambapo limetumika kuuza madafu na bidhaa nyingine huku wala madafu wakiacha vifuu katika eneo hilo na hivyo kutia aibu kutokana na eneo hilo kutumiwa kama njia kuu ya viongozi.
Naye Meneja Uendeshaji wa kampuni ya Green Waste Pro Ltd, Abdallah Mbena amesema kwamba wamefurahishwa na kampeni hiyo kutokana na mabadiliko makubwa yaliyojionesha katika maeneo ambayo wamekuwa wakiyasimamia usafi.
Meneja Kitengo cha Makontena TICTS, Bw. Donald Talawa (kulia), akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na ushiriki wao kwenye zoezi la kusafisha mazingira yanayozunguka fukwe za bahari ya hindi kata ya Kivukoni lililokuwa likiendeshwa na kampuni iliyopewa zabuni ya kusafisha manispaa ya Ilala Green Waste Pro Ltd. Katikati ni Meneja wa mwendeshaji wa kampuni ya Green Waste Pro Ltd, Abdallah Mbena na Kushoto ni Afisa Mtendaji wa Kata ya Kivukoni Bw. Renatus Ruhungu.
Alisema kampeni hiyo imefanikiwa kushawishi wananchi kutambua umuhimu wa usafi na kwamba tabia ya kutupa taka hivyo katikati ya mji sasa imepungua sana.
Pamoja na kushukuru wadau wote walioshiriki katika kampeni hiyo kuanzia manispaa ya Ilala watendaji na wadau wengine wa usafi alisema wananchi wanatakiwa kuendelea kufahamu kwamba suala la usafi ni lao na wala si la makampuni ya usafi pekee.
Aidha aliwataka wananchi kuhakikisha wanalipia huduma za usafi na pia kuwa na vifaa vya kuhifadhia usafi kuanzia katika majumba yao hadi katika mitaa.
Baadhi ya wafanyakazi wa kampuni ya TICTS wakimsikiliza Meneja Kitengo cha Makontena TICTS, Bw. Donald Talawa (hayupo pichani) alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kwenye maeneo ya fukwe za bahari ya hindi zilizopo katika Kata ya Kivukoni.
Afisa Mtendaji wa Kata ya Kivukoni Bw. Renatus Ruhungu akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) ambapo alitoa pongezi kwa kampuni ya Green Waste Pro Ltd kwa kuifanya manispaa ya Ilala kuwa safi na kutaka kampuni zingine za usafi kuiga mfano wa kampuni hiyo na kuwaasa wananchi kutoa ushirikiano wa masuala ya usafi wa mazingira kwa sababu ni jukumu la kila mmoja kuhakikisha mazingira yetu yanayotuzunguka yanakuwa safi wakati wote.
Baadhi ya wafanyakazi wa kampuni ya TICTS na Green Waste Pro Ltd wakishirikiana kusafisha fukwe za bahari ya hindi wakati wa kuhitimisha kampeni ya usafi iliyokuwa ikiendeshwa na Green Waste Pro Ltd.
Kulia ni Meneja uhusiano wa TICTS, Jema Kachota na mfanyakazi mwenzake wakielekea kushiriki zoezi la kusafisha fukwe hizo lililokuwa likiendeshwa na kampuni ya Green Waste Pro Ltd ambapo TICTS nao waliunga mkono kampeni hiyo iliyofikia tamati mwishoni mwa juma.
Meneja Kitengo cha Makontena TICTS, Bw. Donald Talawa (kulia) akivaa glovu tayari kushiriki zoezi la kusafisha mazingira yanayoizunguka bahari ya hindi katika Kata ya Kivukoni mwishoni mwa juma. wengine ni baadhi ya wafanyakazi wa TICTS.
Meneja Kitengo cha Makontena TICTS, Bw. Donald Talawa akishiriki kuzoa uchafu uliotapakaa kwenye fukwe hizo akishirikiana na baadhi ya wafanyakazi wa kampuni ya Green Waste Pro Ltd pamoja na wafanyakazi wenzake.
Umoja ni Nguvu...... wafanyakazi wa kampuni ya Green Waste Pro Ltd wakizoa uchafu uliopo pembezoni mwa fukwe hizo wakati ambao wakati mwingine unapelekea kutoa harufu mbaya kwenye maeneo hayo.
Afisa Rasilimali watu wa kampuni ya Green Waste Pro Ltd, Naima (kushoto) akishiriki zoezi hilo na wafanyakazi wenzake wa kampuni hiyo.
Pichani juu na chini ni wafanyakazi wa Green Waste Pro Ltd wakiendelea kuchapa kazi wakati wa kuhitimisha kampeni yao iliyoungwa mkono na kampuni ya TICTS.
Kwa picha zaidi ingia hapa
regards,
0 Comments