Mamlaka nchini Uturuki zimefunga baadhi ya mipaka yake na nchi ya Syria kwa mara nyingine baada ya takriban watu elfu sabini jamii ya kikurdi kutoka nchini Syria kuingia uturuki wakiwakimbia wanamgambo wa Islamic State.
Siku ya jumapili kulikua na mapigano kati ya vikosi vya usalama na wapiganaji wa kikurdi walikuwa wamekusanyika katika eneo la mpaka wakiwatafuta ndugu zao miongoni mwa wakimbizi.

Jamii nyingine ya kikurdi ilijaribu kuvuka hadi nchini Syria ili kujiunga kupambana na wanamgambo ambao wanaelezwa kuwa wamejisogeza karibu na mji wa Kobani.