Amiri Jeshi Mkuu Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisaini kitabu cha Maombolezo wakati wa kuaga mwili wa Marehemu Meja Jenerali Aidan Isidore Mfuse katika hospitali kuu ya JWTZ ya Lugalo jijini Dar es Salaam jana Novemba 1, 2014  kabla ya mwili huo kusafirishwa kwenda Njombe kwa mazishi yanayotarajiwa  kufanyika leo Jumapili Novemba 2, 2014.

Amiri Jeshi Mkuu Rais Jakaya Mrisho Kikwete akitoa heshima zake za mwisho na kuaga mwili wa  Marehemu Meja Jenerali Aidan Isidore Mfuse katika hospitali kuu ya JWTZ ya Lugalo jijini Dar es Salaam.

Amiri Jeshi Mkuu Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiifariji familia ya marehemu  wakati wa kuaga mwili wa Marehemu Meja Jenerali Aidan Isidore Mfuse katika hospitali kuu ya JWTZ ya Lugalo jijini Dar es Salaam jana Novemba 1, 2014  kabla ya mwili huo kusafirishwa kwenda Njombe kwa mazishi yanayotarajiwa  kufanyika leo Jumapili Novemba 2, 2014.

Mkuu wa Majeshi Jenerali Davis Mwamunyange akiifariji familia ya marehemu  wakati wa kuaga mwili wa Marehemu Meja Jenerali Aidan Isidore Mfuse katika hospitali kuu ya JWTZ ya Lugalo jijini Dar es Salaam.

Rais Mstaafu Mhe Benjamin William Mkapa akitoa heshima za mwisho wakati wa kuaga mwili wa  Marehemu Meja Jenerali Aidan Isidore Mfuse katika hospitali kuu ya JWTZ ya Lugalo jijini Dar es Salaam  leo Novemba.

Waziri wa Ulinzi Dkt Hussein Mwinyi na Waziri wa Ujenzi Dkt John Pombe Magufuli wakitoa heshima zao za mwisho wakati wa kuaga mwili wa Marehemu Meja Jenerali Aidan Isidore Mfuse katika hospitali kuu ya JWTZ ya Lugalo jijini Dar es Salaam.

Amiri Jeshi Mkuu Rais Jakaya Mrisho Kikwete, Rais Mstaafu Mhe Benjamin William Mkapa, Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dkt Hussein Mwinyi, Waziri wa Ujenzi Dkt John Pombe Magufuli, Mkuu wa Majeshi Jenerali Davis Mwamunyange na Mnadhimu Mkuu wa JWTZ Luteni Jenerali Samuel Ndombe wakati wa  kuaga mwili wa Marehemu Meja Jenerali Aidan Isidore Mfuse katika hospitali kuu ya JWTZ ya Lugalo jijini  Dar es Salaam.