Jaji Warioba akitolewa nje ya ukumbi wa Ubungo Plaza jijini Dar chini ya ulinzi mkali baada ya vurugu kutokea .
VURUGU zilizoambatana na ngumi kurushwa zimetokea jana katika Ukumbi wa Ubungo Plaza jijini Dar es Salaam wakati aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Warioba alipokuwa akitoa mada kwenye mdahalo wa kujadili umuhimu wa kuielewa kwa kina Katiba inayopendekezwa kama ilivyopitishwa na Bunge Maalum la Katiba.
Vurugu hizo zimezuka baada ya watu waliokuwa na mabango kuvamia ukumbuni hapo na kusababisha baadhi ya watu waliokuwa wanafuatilia mdahalo huo kuwakabili na kuwapa kichapo.
Baada ya vurugu hizo, mdahalo huo ulioandaliwa na Taasisi ya Mwalimu Nyerere na kurushwa moja kwa moja na ITV umesimamishwa kwa muda.