Askari akitaka kuona leseni ya bodaboda.
Jamaa akijitayarisha kutoa leseni.

Hapa vibali vinakaguliwa.

Pikipiki ya ubalozi nayo ilinaswa ‘kibahati mbaya’ katika msako huo.

Anachomoa leseni kwa mbwembwe.
Jeshi la polisi jijini Dar es Salaam kwa kushirikiana na askari wa ulinzi shirikishi leo limeonekana kushikia bango agizo la kuzikamata pikipiki zisizokuwa na kibali cha kuingia maeneo ya mjini hasa maeneo ya Kariakoo, Posta, Jangwani, Karume, na sehemu nyinginezo. Mtandao huu ulikuwa mitaani na kunasa picha kadhaa kuhusu tukio hilo maeneo ya Posta jijini Dar.