Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe.
Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe ametimiza miaka 91 jana.
Mugabe amekuwa ni kiongozi mzee kabisa duniani kwa kuwa madarakani kwa miaka 35.
Sherehe ya siku yake ya kuzaliwa inategemewa kufanyika wiki ijayo katika Uwanja wa Golf, Victoria Falls.
Sherehe hiyo ambayo itakuwa kubwa na kuhudhuriwa na maelfu ya watu, inaelezwa kugharimu kiasi cha dola milioni moja.