Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Hawa Ghasia akitoa hutuba yake wakati wa uzinduzi wa bodi mpya ua wadhamini ya Mfuko wa Pensheni wa LAPF Dar es Salaam jana.
 Waziri wa Kazi na Ajira Gaudentia Kabaka akichangia jambo kwenye uzinduzi huo.
 Mkurugenzi Mkuu wa LAPF, Eliud Sanga akizungumza machache kwenye uzinduzi huo.
 Mwenyekiti wa Bodi ya Udhamini wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF Profesa, Hasa Mlawa (kulia), akimkabidhi Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Hawa Ghasia picha yenye nembo ya mfuko huo kwenye  hafla ya uzinduzi wa bodi mpya ya wadhamini ya mfuko wa LAPF na kuiaga bodi iliyomaliza muda wake iliyofanyika makao makuu ya mfuko huo Dar es Salaam jana. 
 Mwenyekiti wa Bodi ya Udhamini wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF Profesa, Hasa Mlawa (kulia), akimkabidhi Waziri wa Kazi na Ajira Gaudentia Kabaka picha yenye nembo ya mfuko huo kwenye  hafla ya uzinduzi wa bodi mpya ya wadhamini ya mfuko wa LAPF na kuiaga bodi iliyomaliza muda wake iliyofanyika makao makuu ya mfuko huo Dar es Salaam jana. Kushoto ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Hawa Ghasia.
 Wajumbe wa bodi ya LAPF iliyomaliza muda wake.
 Wajumbe wapya wa bodi ya LAPF 
 Mgeni rasmi wa uzinduzi huo Waziri Hawa Ghasia (katikati mbele waliokaa), akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa bodi ya zamani ya LAPF iliyomaliza muda wake. Kushoto kwa waziri Ghasia ni Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudentia Kabaka ambaye wizara yake inasimamia mifuko hiyo ya kijamii.
 Mgeni rasmi wa uzinduzi huo Waziri Hawa Ghasia (katikati mbele waliokaa), akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wapya wa  bodi ya LAPF.
 Wageni waalikwa wakiwa kwenye uzinduzi huo.
Wadau wakiwa kwenye hafla hiyo
Wanahabari wakichukua taarifa za uzinduzi huo.
Dotto Mwaibale
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Hawa Ghasia ameitaka bodi mpya ya Mfuko wa LAPF kufanyakazi zao kwa maslahi ya mfuko huo badala ya kupendelea taasisi walizotoka.
Hayo aliyasema wakati  wa hafla ya uzinduzi wa bodi mpya ya wadhamini ya mfuko wa Pensheni wa LAPF na kuiaga bodi iliyomaliza muda wake iliyofanyika makao makuu ya LAPF  Dar es Salaam jana. 
" Bodi hii mpya imeundwa katika mfumo wa utatu. Kwanza kuna wajumbe ambao wanatoka serikalini, pili wanaotoka chama cha waajiri, na tatu wajumbe kutoka vyama vya wafanyakazi hivyo ninyi wajumbe.
 mna hadhi sawa katika utoaji michango itakayosaidia kuboresha shughuli za Mfuko" alisema Ghasia. 
Ghasia alisema wajumbe hao wote shughuli yao na lengo lao ni moja, nalo ni kusimamia malengo na kazi za mfuko na kuhakikisha wanaasimamia maslahi ya mfuko na siyo eneo ambako kila mmoja wao anatoka. 
 “Kwa maneno mengine msifanye kazi kimajimbo”, kwani kufanya hivyo, kutaleta migongano isiyo na tija na kuzorotesha ustawi wa mfuko, ambao kwa sasa ndio mfuko wa hifadhi ya jamii unaokua kwa kasi zaidi nchini" alisema Ghasia.
Alisema anaamini wajumbe hao wote wameteuliwa kwa nia moja moja ya kuhakisha mfuko huo unaongezeka hadi kufikia kilele cha mafanikio cha kuigwa hapa nchini na pengine nje ya nchi na hiyo ndiyo imani kubwa ambayo Rais Jakaya Kikwete anayo kwa LAPF.
Mwenyekiti wa Bodi ya Udhamini wa mfuko huo Profesa, Hasa Mlawa alisema michango ya wanachama imekuwa ikiongezeka pia kwa kiwango cha kuridhisha ambapo mwaka 2011 mfuko ulikusanya Sh. 80.5 bilioni na kiasi hicho kimeongezeka hadi kufikia Sh. 157.6 bilioni mwezi Juni 2014 sawa na ongezeko la asilimia 95.9 kwa kipindi cha miaka mitatu. 
Alisema mambo yaliyofanya kiwango cha michango kuwa juu ni pamoja na ongezeko la wanachama, mishahara, na uwasilishaji wa wakati unaofanywa na waajiri na kuwa kutokana na michango hiyo fedha zilizowekezwa katika vitegauchumi mbalimbali nazo ziliongezeka toka Sh. 387.6 bilioni mwezi Juni 2011 hadi Sh. 748.67 bilioni mwezi Juni 2014 sawa na ongezeko la asilimia 93.2. 
Waziri wa Kazi na Ajira Gaudentia Kabaka ambaye mifuko hiyo ya jamii ipo chini ya wizara yake alisema Serikali itaendelea kulipa madeni yanayodaiwa na mifuko hiyo ili kuifanya iweze kuendelea.