Raisi wa Marekani Barack Obama
Raisi Barack Obama ametoa mwito kwa wa Nigeria kusitisha vurugu hasa kuelekea uchaguzi mkuu wa nchi hiyo mapema mwishoni mwa wiki hii.
Wasi wasi wa hali ya usalama umezidi kuongezeka nchini humo wakati siku ya kupiga kura kadiri inavyokaribia ambapo wananchi wa Naijeria wanatarajiwa kupiga kura jumamosi wiki hii baada uchaguzi huo kuhairishwa mwezi uliopita kutokana na mashambulio ya kundi la Boko Haram.

Rais Obama amesema kwamba Nigeria inapaswa kufanya uchaguzi ulio huru na wa haki.
wanaijeria wote wanapaswa kupiga kura zao bila ya vitisho ama wasi wasi .Hivyo natoa wito kwa viongozi wote pamoja na wagombea kuzungumza na wapiga kura wao kwamba vurugu hazina nafasi katika uchaguzi wa kidemokrasia,na hawapaswi kuchochea, wasaidie au kujihusisha na vurugu zozote kabla ama baada ya uchaguzi na wakati wa kuhesabu kura.
Nina waomba wanaigeria wote kueleza hisia zenu kwa amani na kuwapuuza wote wanaotoao wito wa kufanya vurugu .
Wakati Rais Obma akitoa wito huo Joto la uchaguzi linazidi kupamba moto nchini Nigeria.
Mvutano mkali upo kati ya rais Goodluck Jonathan wa chama tawala cha PDP na mgombea wa upinzani Jenerali Muhhamadu Buhari wa APC. Wananchi wa Nigeria watapiga kura siku ya Jumamosi kuchagua mtu atakayewaongioza kwa miaka minne ijayo.