Ajali imewaua watu 31 nchini Morocco wengi wao wakiwa wanariadha vijana
Ajali ya ana kwa ana kati ya basi na lori nchini Morrocco imewaua watu 31 wengi wao wakiwa wanariadha vijana ,kulingana na maafisa.
Wanariadha tisa wameripotiwa kujeruhiwa karibu na mji wa kusini wa Tan-Tan.

Wengi wa waathiriwa waliuawa baada ya moto kulichoma basi hilo wakati wa ajali,kulingana na vyombo vya ahabari vya eneo hilo.
Ajali hiyo inadaiwa kutokea katika barabara kati ya mji mkuu wa Rabat na Laayoune ambao uko magharibi mwa Sahara.
Ilitokea mapema siku ya ijumaa katika wilaya ya mashambani ya Chbika karibu na Tan -Tan kulingana na vyombo vya habari vya eneo hilo.
Wengi wa wale waliokuwa wakiabiri basi hilo walikuwa wanafunzi waliokuwa wakishiriki katika mashindano ya michezo kulingana na mtandao wa le360.ma