Zaidi ya watu kumi wameuawa katika msururu wa ghasia viungani mwa mji mkuu wa Libya Tripoli.
Ghasia hizo kutoka maeneo mawili zilikuwa kati ya wanamgambo walio watiifu kwa serikali ya tripoli na wale walio watiifu kwa serikali inayatombuliwa na jamii ya kimataifa iliopo mashariki mwa taifa hilo.
Milipuko ya mabomu ya mara kwa mara pamoja na milio ya risasi imesika katika eneo la Fashloum ambapo baadhi ya watu wamekamatwa na wapiganaji walio watiifu kwa serikali ya Tripoli
0 Comments