MASIKITIKO! Baada ya mrembo Wema Sepetu kutupia ujumbe kupitia mtandao wa Instagram kuwa si kwamba hapendi kuzaa bali hana uwezo wa kufanya hivyo mashabiki wake wengi wameonekana kuumizwa na taarifa hiyo.
Wengi wa mashabiki wameonekana kumpa ple Wema na kumtia moyo kuwa ipo siku naye atapata mtoto na kuitwa mama.
Wema aliamua kuandika ujumbe huo baada ya kushambuliwa na baadhi ya mashabiki wasiomtakia mema alipompongeza mwanamitindo Hamisa Mobeto aliyejifungua hivi karibuni.
Hizi ni meseji za baadhi ya mashabiki waliomtia nguvu Wema...
Ujumbe aliouandika Wema Sepetu huu hapa:
Ujumbe aliouandika Wema Sepetu huu hapa:
Ningekuwa na uwezo wa kuzaa ningekuwa nimezaa muda mrefu sana... But sina... Na siwezi kumkufuru mwenyezi mungu.... Au mngependa niwe nawaambia jinsi ninavyo hangaika usiku na mchana kupata mtoto wangu mwenyewe... Is dat wat u want...? kila ntakachofanya kwa ajili ya tumbo langu basi nitangaze... Au mnadhani siumii mnavyosema kuhusu maswala ya mtoto... Kumbukeni na mimi pia ni binaadam... Nina moyo kama nyie... Au mnadhani napenda kuona wenzangu wana watoto au wana ujauzito alafu mimi sina hata wa kusingiziwa... Mnaona nafurahia sio.... Hivi mna nini jamani...
Yaani mtu unaweza weka post kwa nia nzuri then people jus come from nowea wanaanza kukuandikia maneno ya kukuumiza kabisa nafsi hadi mtu unakaa unajiuliza umemkosea nini mwenyezi Mungu... Kwani kuna niliemkosea yoyote mpaka muanze tu kunikashif na kunitolea maneno mazito namna hio... Kisa mtoto... Mnadhani naipenda hii hali... Hata mimi natamani kuitwa mama na hakuna kinachoniuma kama hicho....
So mnadhani sijui kama umri unaenda na maisha yenyewe sikuhizi mafupi anytime we die... Mnafikiria nisingependa kuacha hata ka copy kangu siku ndo Mungu anasema ananichukua... Hata mimi natamani ningekuwa napiga picha niko na mwanangu... I want dat with all my life but I cant.... Sitokaa nimkufuru Mungu wangu hata siku moja maana sijui ni kitu gani kaniandikia... But just dont rub it in... It hurts... And im jus a human being like each and everyone of u....
Ujumbe aliouandika Wema akimtakia heri Hamisa Mobeto na kupelekea ashambuliwe kwa matusi:
They say u are nat yet a woman Until you experience motherhood........ By da way who are they who keep saying things everytime... They always have something to say dont they..? Lol... Back to reality... Jamani my mdogo umezaa...! I just heard you were pregnant... Oh my...! Hongera mamy.... You are a Woman now....! Cant even start to tell u how much i envy you ryt now... Congratulations either way.... Lotsa kisses to the beautiful lil angel...... @hamisamobetto @hamisamobetto @hamisamobetto Awwwwwww look at you.....
0 Comments