Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (katikati) akimsikiliza Mwakilishi
Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini, Alvaro Rodriguez (kulia), wakati kiongozi 
huyo alipomtembelea Waziri huyo ofisini kwake jijini Dar es Salaam leo, kujadiliana masuala 
mbalimbali ya ushirikiano kati ya Wizara yake na ofisi ya Umoja wa Mataifa (UN) nchini. 
Kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Wakimbizi wa Wizara hiyo, Harrison Mseke, anayefuata ni 
Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Kimataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR) nchini, Joyce 
Mends-Cole.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (kushoto) akizungumza na Mwakilishi
Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini, Alvaro Rodriguez kuhusu masuala
mbalimbali ya ushirikiano kati ya Wizara yake na ofisi ya Umoja wa Mataifa (UN) Tanzania.
Rodriguez alimtembelea Waziri Chikawe ofisini kwake jijini Dar es Salaam leo. Picha zote na
Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.