Mshambuliaji wa Yanga Amissi Tambwe akishangilia baada ya kufunga bao la kwanza dhidi ya Polisi Moro kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar.
Wachezaji wa timu ya Yanga.
YANGA SC imefanikiwa kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom kwa kuifunga Polisi Morogoro mabao 4-1 kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar, licha ya kuwa imesaliwa na mechi kadhaa kumaliza msimu wa 2014/2015. Wafungaji wa mabao ya Yanga leo ni Amiss Tambwe aliyefunga hat trick na Simon Msuva.
KIKOSI CHA YANGA: Dida, Abdul, Joshua, Twite, Yondani, Juma, Msuva, Niyonzima, Tambwe, Ngassa, Sherman.
KIKOSI CHA POLISI MORO: Abdul, Teru, Mganga, Abel, Kambole, Selemani, Bantu, Mkangu, Bahanuzi, Kassim, Ambrose.