Polisi wakiwa katika mitaa ya Misri
Jaji wa mahakama moja nchini Misri ameamuru polisi aliyepelekwa mahamani hapo kwa tuhuma za kumua mwanamke mmoja mwanaharakati wakati wa maandamano mwezi Januari awekwe mahabusu. Tukio hilo lilisababisha ghasia kubwa nchini humo baada ya video yenye kuonesha kifo cha mwanahati huyo kusambazwa katika mitandao ya kijamii.

Shaimaa el-Shabbagh alikufa baada ya kupigwa risasi na askari aliyekuwa ameuficha uso wake,wakati wa maandamano ya amani katika mji mkuu wa nchi hiyo Cairo mwezi January mwaka huu .
Picha video iliyowasilishwa mahakamani na upande wa mashtaka inamwonyesha askari huyo aliyeuficha uso wake akifyatua risasi upande wa mwanamke huyo kabla hajabadilisha silaha hiyo na kubeba kifyatua bomu la machozi.
Kuna madai pia mamlaka zilizuia gari la wagonjwa kuingia ili kumpa huduma muandamanaji huyo aliyekuwa taabani.
Polisi nchini Misri kwa muda mrefu wamekuwa ikikana askari wake kutumia risasi za moto dhidi ya waandamanaji licha ya kuwepo kwa ushahidi mzito unaonyesha wakifanya hivyo.