Diva wa muziki wa Pop nchini Marekani, Beyonce Knowles.
NEW YORK, Marekani
DIVA wa muziki wa Pop nchini Marekani, Beyonce Knowles, amewapa pole wafiwa wa tukio la mauaji ya risasi ya watu 9 yaliyofanywa na kijana, Dylann Roof ndani ya Kanisa la Charleston, South Carolina, wiki iliyopita.
Kijana aliyesababisha mauaji hayo Dylann Roof akiwa chini ya ulinzi.
Kuonesha kuguswa na msiba huo wa kitaifa, juzikati, Beyonce aliweka picha na ramani ya Kanisa la Charleston na majina ya marehemu wote kwenye ukurasa wake wa Instagram huku akiisindikiza na kipande cha video akizungumza maneno ya kuzifariji familia hizo za wafiwa.
“Moyo wangu upo juu ya familia zilizopoteza wapendwa wao na wale wote walioathiriwa na tukio la kusikitisha la Charleston. Marehemu wote wapumzike kwa amani,” alisema Beyonce katika kipande cha video hiyo.