Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue, akiweka saini kwenye Kitabu cha Wageni Ofisini kwa Balozi wa Tanzania, Uingereza, jijini London mwishoni mwa juma.

 Katibu Mkuu Kiongozi, Mheshimiwa Ombeni Sefue, akizungumza na Maafisa wa Ubalozi, alipotembelea Ubalozini hapo. Mheshimiwa Katibu Kiongozi alikuwa nchini Uingereza katika Ziara yake ya kikazi ambayo iliandaliwa na Taasisi ya ESAMI kuhudhuria semina ambayo ilikuwa na lengo la kuwakutanisha Viongozi wa Vyama vya Siasa na Watendaji wa Serikali, kuangalia changamoto mbalimbali ambazo wanakumbana nazo na muingilio wake katika utendaji wa kazi zao za kila siku.

 Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue akiwa pamoja na Balozi wa Tanzania, Uingereza, Mhe. Balozi Peter Kallaghe, kwenye Ofisi za Ubalozi Tanzania London, Uingereza.

Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue (waliokaa-kushoto) na Balozi wa Tanzania Uingereza, Mhe. Peter Kallaghe (waliokaa-kulia), wakiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya Maafisa wa Ubalozi. Mheshimiwa Katibu Mkuu Kiongozi alitembelea ofisi hizo za Ubalozi na kupata nafasi ya kuzungumza na Maafisa hao mara baada ya kumaliza ziara yake ya kikazi nchini Uingereza. Picha na Rashid Dilunga