MSOMI mwenye shahada ya pili ya uongozi na Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana CCM (UVCCM), mkoa wa Rukwa, Philipo Elieza amechukua fomu ya kuomba ridhaa ya kuwania nafasi ya ubunge katika jimbo la Mtera ambalo kwa sasa linaongozwa na Livingston Lusinde.Kada huyo amesema amelazimika kurudi nyumbani kuwatumikia wananchi kutokana na wakazi wa mtera kukabiliwa na changamoto mbalimbali kwa kukosekana mtetezi wa kweli katika masuala ya kimaendeleo.
Amesema mbali na kukosekana kwa maendeleo amesema Jimbo la Mtera kwa sasa limekuwa na vijana ambao wamejengewa chuki ya kuchukiana wao kwa wao na kufikia hatua ya kupigana na jureruhiana jambo ambalo limaondaoainami ya watanzania kwa Chama cha Mapinduzi (CCM).
“Inasikitisha sana kuona vijana wa jimbo moja wakitengeneza makundi kwa ajili ya kugombana wao kwa wao, kisa wanagombanishwa na kiongozi ambaye alitakiwa kuwaunganisha”amesema Elieza.
Amesema umefika wakati wa vijana kuachana na tabia ya kutumiwa na wanasiasa kwa ajili ya kufanya siasa za chuki, kupigana na kuumizana na kutoana damu.
Amesema katika uchaguzi unaokuja kwa vyama vyote ni vyema siasa zikaendeshwa kistaarabu pamoja na kujenga hoja badala ya kutukanana na kukashifiana jambo ambalo halipendezi na alimfurahishi Mwenyezi Mungu.
Pamoja na kutowataja watu ambao wanachochea fujo katika jimbo hilo ni kutokana na kauli ya mbunge wa sasa kuwashawishi vijana kuwapiga vijana wengine ambao hawamuungi mkono.
Kwa mujibu wa taarifa mbalimbali ambazo zilitolewa katika vyombo vya habari zilieleza kuwa Lusinde akiwa katika mkutano wake wa hadhara aliwaangiza vijana ambao wanamuunga mkono kukaa pembeni na wale wasiomuunga mkono wakae pembeni.
Kutokana na hali hiyo Lusinde aliagiza kundi linalomuunga mkono kuwashambulia wale wasiomuunga mkono hata hivyo Lusinde alikanusha tuhuma hizo.
Mbali na kuhimiza amani katika uchaguzi amesema lengo la kuchuka fomu katika kuomba ridhaa ya kuomba kuwania nafasi ya ubunge katika jimbo la mtera ni kutokana na jimbo hilo kukosa maendeleo.
Elieza amesema katika uongozi wa miaka mitano ambayo sasa inaisha bado jimbo hilo limeendelea kuwawa nyuma na mbaya zaidi kumezuka tabia ya viongozi kupandikiza chuki katika makundi ya vijana.
Amesema jambo pekee ambalo mtangaza nia huyo ataanza nalo ni kuhakikisha anawaunganisha vijana ambao kwa sasa wamelifanya jimbo la mtera kuwa sehemu ya mapambano.
“Nijuzi tu vijana walipigana na kutoana ngeu jambo ambalo ni hatari zaidi katika maisha ambayo watanzania wameyazoea.
“Inasikitisha kuona baadhi ya viongozi ambao wanatazamiwa kuwa waunganishi katika jamii kwa maana ya kulinda amani wao wanakuwa wakwanza kuvuruga amani” amesisitiza.
Elieza amesema yapo mambo mengi ya kufanyia wananchi ili wapate maendeleo,ambayo yatawaondoa katika umasikini uliokithiri.
Jambo lingine ambalo Elieza alilizingumzia ni pamoja na kutekeleza ilani ya Chama tawala na kueleza kwamba iwapo atapata ridhaa ya kuwa mbunge wa mtera atahakikisha huduma muhimu zinawafikia wananchi.
Akizungumzia kazi alizozifanya jimboni licha ya kutokuwa Mbunge ni pamoja na kuwatafuta wafadhili na kuiwezesha shule ya msingi ya mvumi kusoma masomo ya Tehama.
Amesema amekuwa mwenyekiti wa shule ya sekondali ya Dk .Samweli Malecela,iliyopo ilolo Mvumi.
Akizungumzia tatizo ambalo linawakumba wanachi wa mvumi alisema ni pamoja na kukosekana kwa huduma muhimu kama vile, Elimu, Afya,Maji mawasiliano pamoja na miundombinu rafiki kwa wananchi.
Kwa upande wake Katibu wa CCM wilaya ya Chamwino,Janeth Mashere, alisema kwa sasa mchakato huo unaendelea vizuri na wapo watu wengi wanaendelea kujitokeza kuchukua fomu.
0 Comments