Shekh Yussuf mwenye kofia ya manjano akifungua dua ya kumrehemu mama mzazi wa Ally Mohammed Mlangi {mwenye kanzu nyeupe} hapo jana kitongojini Mol nchini Ubelgiji.

 Kisomo cha kumrehemu mama wa Ally Mlangi kikiendelea huku kila mmoja akishiriki vyema katika dua
Brother Joseph akishiriki vyema dua

Kitezo kikifuka moshi ni ishara njema kwamba dua inaendelea vyema.Ustadhi Vierra akiendeleza dua

Waungwana walioshiriki jana katika kisomo

Kikosi kazi kikiendelea kuomba dua hapo jana

Selle wa Leuven kulia na kamanda wa msitu mnene pia walishiriki vyema katika dua ya jana

Waungwana kutoka sehemu mbalimbali wakihitimisha dua ya mwisho

Mama Nasreen kushoto akiwa na dada Nasria wa Antwerpen wakipata dua

Dua ikiendelea huku Queen Rahma na mama yeke mama Sarah wakiendelea kuomba dua

Kwa upande wa kina mama nao walishiriki vyema katika dua ya kumrehemu mama wa Ally Mlangi,pichani ni mama Denzel mwenye mtandio mwekundu akiwa na mama yake Mrs Khalid

Naam dua ikiendelea huku pichani Katibu mkuu ndugu Mohammed Mwalimu mwenye jaketi la manjano,akifuatiwa na ndugu Ally Mlangi{muhusika mkuu wa kisomo} na ustadhi Vierra

Brother Gebo akishiriki dua ya kumrehemu mama yake mzazi na Ally aliyetangulia mbele za haki siku chache zilizopita

Brother Zile akishiriki dua na kijana wake pembeni

''Uuungwana na vitendo'' ni kauli nzuri ya wahenga....Pichani ndugu Ally ambaye ni mfiwa wa mama yake akitoa shukrani za dhati kwa kila mmoja aliyeshiriki kwa namna moja au nyingine katika kufanikisha shughuli ya dua ya kumuombea mama yake mzazi aliyetangulia mbele za haki siku chache zilizopita nyumbani Afrika.

Mrs Maganga One [kushoto] akiwa na Mrs Hamza

Mmoja wa waliofika kwenye dua akiwa makini kabisa kusikiliza mawaidha

Queen Rahma na mama Saraha

Shekh Vierra akitoa mawaidha kuwakumbusha wanaadamu kuhusu suala la kifo huku wengine wakionyesha kuguswa kwa namna moja au nyingine

Waungwana wakisikiliza mawaidha kwa hisia kabisa

Mchezaji mkongwe wa timu ya Taifa ya Tanzania Kassim Manara akipata kumbukumbu baada ya dua

Mrs Moddy akisikiliza mawaidha yanayozunguzia kifo huku akionesha hisia zake

Queen la Antwerpen Rahma akiwa na mama yake mama Sarah

kutoka kushoto ni dada Ummy wa Antwerpen,Mrs Maganga One {katikati}  na Mrs Hamza

Bidada Dida akiwasili ukumbini,kamera ikamnasa namna hii

Dida akiwa na mama yake na watoto wake

Pichani ni mama Mansoor,Mansoor na mama Tillah

Masha'Allah watoto wa Hamza nao walishiriki kwenye dua

Dada Khasser[Mrs Yussuf] kushoto akiwa na dada Sharon

Kamanda wa msitu mnene akibadilishana mawazo na dada yetu Khasser

Mama Mansoor akiwa na mtoto wake Msham mara baada ya kisomo

Mama Tillah pia alikuwepo

Taswira endelevu

Kitengo cha madikodiko kilidhibitiwa na Mbabe huyuu

Team Mol ikiwa makini kabisa kuhakikisha kila mmoja anapata huduma stahiki na kwa wakati

Sadak ikiendelea

Sadaka ikitolewa kwa upande wa kina mama

Mrs Dullah akipata sadak

Shekh Yusuf akitoa huduma ya Sadak

Mama Kauthar akipata sadak hapo jana

Kikosi kazi kikiwa tayari kuwajibika 

 Ndugu zetu kutoka Antwerpen nao walishiriki vyema katika shughuli nzima ya dua
Waungwana wakipata Sadaka

Brother Nyambi pia alikuwepo kwenye kisomo cha jana

Dida akiwa na watoto wake katika kisomo cha jana

 Ndugu zetu kutoka sehemu mbalimbali walifika Mol kujumuika nasi katika kisomo
  Ndugu zetu kutoka sehemu mbalimbali walifika Mol kujumuika nasi katika kisomo
 Kila mmoja alijaaliwa kupata sadaka
Brother Zile kushoto na kijana wake na ndugu yetu pia wakipata sadaka mara baada ya dua

Ndugu yetu na mwanawe  wakipata kumbukumbu

Ndugu zetu wakiendelea kupata sadaka

Kada mkuu wa Ukawa nchini Ubelgiji Mussa Mudrik akipata sadaka mara baada ya kisomo

Sele rasta mchezaji bora wa mwaka kutoka Liege nae alishiriki dua ya kumrehemu mama wa Ally Mohammed Mlangi iliyofanyika Mol Ubelgiji

Wakati wa sadak ulipowadia kila mmoja wetu alionekana hiviii

Katika hali ya ushirikiano mwema kwenye shida na raha,hapa unaweza kuwaona ndugu hawa wawili wakipata picha ya  pamoja baada ya dua.

Mara tu baada ya shughuli ya kisomo kuisha,ndugu Ally Mlangi kulia akionyesha hali ya kumshukuru Allah kwamba dua ilikwenda salama kabisaa.

Two Brothers in hood

Muda mchache shughuli ya kisomo ilipokwisha kila mmoja alipata muda wa kusalimiana na mwingine,pichani Kamanda wa msitu mnene akibadilishana mawazo na dada zake wa Mol