3. Thyroid & Parathyroid Gland: imekaa shingoni, na inamiliki mabadiliko ya chakula kilicho liwa mwilini “Metabolism”, na kumiliki kima cha joto mwilini”Body heat”. Hali kadhalika makuzi na uchafu ndani ya mwili. Panapokuwa na kasoro ya udogo au ukubwa wa miliki hii, matokeo yake ni kukasirisha mishipa ya fahamu mwilini na kuwa hoi au kuchoka kila mara. Calcium na phosphorus zinamilikiwa na hii Gland.
4. Thymus Gland: Ipo katika ya kifua, na huwa kubwa mno utotoni na mtoto afikiapo barehe inapungua kuwa robo ya umbo lake. Hii ni silaha ya kinga za mwili kwa mashambulizi ya magonjwa ya nje ndani ya mwili. Ina miliki udumishaji ulinzi wa kupambana na magonjwa nayayo shambulia mwili.
5. Adrenal Glands: Hii ipo juu kidogo ya mafigo, kazi yake hasa ni kutoa nguvu na moto la hali ya juu na kuamua penye jambo la hatari au tukio, hisia ya mwanaadam aidha uamua kukimbia au kupigana kijasili kwa kupambana na tukio lolote.
6. Pancreas: ipo chini kidogo ya tumbo na kazi yake ni kuyeyusha kemikali ijulikanoyo kama “Enzyme”. Katika utumbo mdogo, inachanganya “Insulin” hormone inayo punguza nguvu za sukari katika damu. Endapo Pancreas inashindwa kumiliki vyema utengenezaji wa Insulin mwilini, basi sukari ya damu huimalika Zaidi katika mwili na matokeo yake ni Diabetes mellitus au ugonjwa wa kisukari. Pia papo hapo, Insulin nyingi nayo sio nzuri, husababisha kutetemeka na udhaifu mwilini.
7. Gonards: Uume au uuke, na kazi yake ni kumiliki kazi ya ngono. Zina changanya Endrogen ambayo ni hormone ya jinsia ya kiume, pia Estrogen kwa wanawake. Hizi zote zinafanya kazi ya tabia ya mwili wa kike na kiume kwa jinsia zilivyo tofautiana.
Maumbile ya mwili mzima wa mwanaadam , inamilikiwa na hizo Hormones. Hapo ndipo utakuta, kupitia mazoezi ya aina ya “ Yoga Asanas”, mwili unaweza kumiliki na kusawazisha mzani wenye kima cha wastani katika uchanganyaji wa hizo hormones mwilini.
Mafunzo ya mazoezi ya Yoga, yanadhihirisha wazi kutokana na masomo mbalimbali ya uchunguzi toka vyuo vikuu vingi maarufu nchini Marekani na kuandikwa kwa majarida mbali mbali yenye malengo ya kuielimisha jamii kuhusu afya na maumbile kupitia mazoezi ya Yogasanas.
Imeandikwa na mwalimu wa Yoga, Rumadha Fundi kupitia majarida ya chuo alicho somea filosofia ya Yoga cha “College of Neo Humanist Studies”, Gullringen, Sweden na pia Tiljala, Culcutta, West Bengal, India ’87.
Sensei Rumadha Fundi , Yoga & Karate Instructor.
0 Comments