Shoga moro (2)Kijana Karimu Said ‘Anti Karim’ akitoa ushuhuda redioni.
STORI: Dustan Shekidele, Ijumaa Wikienda
Morogoro: My confession! Katika hali isiyo ya kawaida, kijana Karimu Said (25) almaarufu Anti Karimu aliyekiri kufanya biashara haramu ya kuuza mwili (ushoga), ameangua kilio redioni wakati akiutangazia umma wa Watanzania kuachana na dhambi hiyo aliyodumu nayo kwa miaka saba.

Shoga moro (1)Anti Karim akiendelea kufunguka.
Ilikuwa Alhamisi iliyopita, Karimu alifika katika ofisi ndogo za gazeti hili za mkoani hapa na baadaye alitinga kwenye Kipindi cha Mcharuko wa Pwani cha Radio Planet FM kinachoendeshwa na mtangazaji mahiri, Warda Makongwa akishirikiana na Farham Abraham.
Lengo la Karimu lilikuwa ni kutubu dhambi yake hiyo sambamba na kumuomba msamaha Mwenyezi Mungu na Watanzania kwa jumla.
Akiwa hewani laivu kwenye kipindi hicho na watangazaji hao na mwandishi wetu, Karimu alisimulia kilichomwingiza kwenye ushoga kuwa ni umaskini uliotokana na vifo vya wazazi wake.
Shoga moro (3)“Baada ya wazazi wangu kufariki dunia na mimi kumaliza darasa la saba hapa Morogoro, nilikwenda Dar kutafuta kazi. Nilipofika nilipata kazi ya ndani (house boy) kwa bosi mmoja.
“Nikiwa hapo, bosi wangu wa kike na wanaye walikwenda likizo kijijini, mimi nilibaki na bosi wa kiume.
“Siku moja huyo mwanaume alinirubuni akanipeleka beach (ufukweni) na baadaye Mlimani City ambako alinilazimisha kunywa pombe.
“Tuliporudi nyumbani aliniingilia, tangu hapo kila siku akawa akinifanyia hivyo. Mkewe aliporudi alinikanya nisimwambie, nikajikuta namuonea wivu huyo mwanaume hata akiwa na mkewe.
Shoga moro (4)
“Hali hiyo ilisababisha mkewe kujua na kunitimua,” alisema Karimu.
Alisema kuwa baada ya kutimuliwa alirejea kwao Morogoro na kuendelea na ushoga akijiuza kwenye madanguro yaliyopo ltingi na Kahumba mjini hapa.
Alipoulizwa wateja wake wakubwa ni watu gani, Karimu alifunguka kuwa ni waume za watu wakiwemo baadhi ya vigogo wa serikali.
Mwandishi wetu alipomtaka kuelezea changamoto alizokumbana nazo, alifunguka huku akiangua kilio studio: “Changamoto ni nyingi zikiwemo za kupigwa, kupata bwana akakulipa elfu arobaini lakini ukifika geto kwake, ukishamhudumia, anakugeuka na kukunyang’anya fedha.
“Nimeyatafakari matukio yote hayo, ndipo nikaungana na rafiki yangu aliyenipeleka kanisani ambako niliombewa hadi nikaanguka, nikapoteza fahamu, nilipozinduka nikajiona niko kwenye ulimwengu mwingine na kujutia dhambi hiyo ya ushonga, hivyo naomba Mungu na Watanzania wanisamehe,” alisema Karimu huku akilia.
TAZAMA VIDEO AKISIMULIA