Aliyekuwa mkewe rais mwazilishi wa Afrika Kusini Nelson Mandela na shujaa wa ukombozi bi Winnie Madikizela-Mandela amelazwa katika hospitali moja ya Johannesburg,baada ya kufanyiwa upasuaji wa dharura.
Bi Winnie Madikizela anauguza majeraha ya mgongo.

Madaktari walimfanyia upasuaji wa kwanza tarehe 8 mwezi Machi baada ya uchungu kumzidia.
Hata hivyo hali yake haikuimarika na hivyo akalazimika kufanyiwa upasuaji wa pili tarehe 14 Aprili.
Familia yake kwa taarifa waliotuma kwa vyombo vya habari wanawashukuru wale wote wanaoungana nao wakati huu mgumu wa ugonjwa na wanaomba haki yake ya usiri uheshimiwe.
Habari zinawadia juma moja tu baada ya mahakama kuu ya Afrika Kusini kumnyima haki ya kurithi makao ya aliyekuwa rais hayati mzee Nelson Mandela.