Waziri Mkuu wa Uingereza, David Cameron, ametangaza takwimu za mapato yake na kodi aliyotozwa katika kipindi cha miaka 6 iliyopita kufuatia kashfa ya nyaraka za Panama.
Ni mara ya kwanza kwa waziri mkuu aliyeko mamlakani kufanya hivyo nchini Uingereza..

Bwana Cameron amekuwa akikosolewa tangu nyaraka hizo za siri kufichuka kutoka Panama zinazoeleza kuwa baba yake alianzisha wakfu na kampuni ya hewa nchini Panama.
Image copyrightAP
Image captionAlikiri kuwa aliuza hisa kadhaa za wakfu huo na kupata dola za Marekani $44,000 kabla kuchaguliwa kuwa waziri mkuu.
Alikiri kuwa aliuza hisa kadhaa za wakfu huo na kupata dola za Marekani $44,000 kabla kuchaguliwa kuwa waziri mkuu.
Takwimu hizo zinaonyesha kuwa Bw Cameron alipokea jumla ya Dola 300,000 za Marekani kutoka kwa mama yake mwaka 2011, muda mfupi baada ya yeye kurithi dola 44,000 kutoka kwa baba yake.