Mwanamuziki Chris Brown amesema kuwa alitaka kujiua baada ya kumshambulia aliyekuwa mpenziwe Rihanna kabla ya tuzo za Grammy mwaka 2009.
Katika kipande kifupi cha makala yake ya 'Karibu katika maisha yangu',mwanamuziki huyo wa mtindo wa R & B amesema kuwa uhusiano wao ulikuwa kama ndoto lakini akajihisi kama hayawani.
''Nilikuwa katika kilele cha dunia,nyimbo zangu zikiongoza,nikapendwa na wengi nchini Marekani kabla ya kuanguka hadi kuwa adui wa uma'',alisema.
Brown alihukumiwa kifungo cha miaka mitano jela kufuata shambulio hilo.
Kifungo hicho kilisitishwa mwaka jana baada ya jaji moja kusema kuwa nyota huyo amekamilisha mahitaji yake yote na kufunga kesi hiyo rasmi.
Makala hiyo inayowaonyesha Jennifer Lopez,Usher,Mike Tyson,Jamie Fox na Rita Ora,Chris Brown anasema kuwa ''Nilihisi kama nyota ,lakini nilijiharibia''.
0 Comments