Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amewaapisha Makatibu Tawala wapya kumi aliowateua tarehe 25 Aprili, 2016 na kuwapangia vituo vyao vya kazi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  akimuapisha ndugu Albert Gabriel Msovela kuwa katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga Ikulu jijini Dar es salaam Aprili 27, 2016.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  akimuapisha ndugu Amantius Casmiri Msole kuwa katibu Tawala wa Mkoa wa Kagera Ikulu jijini Dar es Salaam Aprili 27, 2016
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  akimuapisha ndugu Angelina Mgeni Lutambi kuwa katibu Tawala wa Mkoa wa Singida Ikulu jijini Dar es Salaam Aprili 27, 2016.
Makatibu Tawala hao wameapishwa leo tarehe 27 Aprili, 2016 Ikulu Jijini Dar es salaam na kisha wametia saini hati ya ahadi ya uadilifu kwa viongozi wa umma, zoezi lililoendeshwa na Kamishna wa maadili Sekreatieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Mheshimiwa Jaji Salome Kaganda na kushuhudiwa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi.
Makatibu Tawala walioapishwa ni;
  1.     Arusha –         Richard Kwitega
  2.     Geita –             Selestine Muhochi Gesimba
  3.     Kagera –          Armatus C. Msole
  4.     Kilimanjaro – Eng. Aisha Amour
  5.     Pwani –           Zuberi Mhina Samataba
  6.     Shinyanga –    Albert Gabriel Msovela
  7.     Singida –         Dr. Angelina Mageni Lutambi
  8.     Simiyu –          Jumanne Abdallah Sagini
  9.     Tabora –         Dkt. Thea Medard Ntara
  10.     Tanga –           Eng. Zena Said
Makatibu Tawala wengine wa Mikoa ambao hawakuapishwa leo, ni wale waliohamishwa vituo vya kazi na wale waliobaki katika vituo vya kazi walivyokuwep,o ambao tayari walishakula kiapo cha kuwa Katibu Tawala wa Mkoa.
Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es salaa
27 Aprili, 2016