Ubelgiji imempeleka mshukiwa wa shambulio la Paris Salah Abdesalam nchini Ufaransa.
Alijeruhiwa na kukamatwa katika operesheni iliofanywa na maafisa wa polisi mjini Brussels baada ya kutoroka kwa miezi minne.
Raia huyo wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 26 alizaliwa mjini Brussels na aliishi mjini humo kabla ya shambulio la Paris.
Takriban watu 130 waliuawa na wengine wengi kujeruhiwa katika mashambulizi ya kupangwa yaliotekelezwa na kundi la Islamic State mjini Paris mnamo tarehe 13 mwezi Novemba.
|
0 Comments