Utawala wa serikali ya kidini katika mji mkuu wa Tripol nchini Libya umekabidhi mamlaka kwa baraza la umoja wa mataifa. Uamuzi huo ulichapishwa katika mtandao wa wizara ya sheria.
Mamlaka mpya ya Libya wiki iliyopita imehamia mji mkuu,Tripol katika harakati za kutaka kutawala nchi nzima, huku kukiwa na ngome nyingine mbili tofauti za utawala Mashariki mwa nchi hiyo.
Tamko hilo limetolewa kwa niaba ya serikali ya kidini inayoushikilia mji mkuu wa Libya Tripol, ambapo hatua iliyofikiwa ni kuvunja baraza lake ili kuweka mbele maslahi ya taifa na kuzuia umwagikaji wa damu.
Hatua hii ni matokeo ya jitihada za umoja wa mataifa kuunda serikali ya pamoja ili kuweza kuondoa mgawanyiko wa utawala ndani ya taifa hilo ulioanza kushamiri tangu wakati wa machafuko mara tu baada ya kuangushwa kwa utawala uliokuwepo.
Serikali ya Libya haijawahi kutambuliwa na jumuiya za kimataifa tangu iingie madarakani mwaka 2014 ambapo utawala mwingine ulijitenga na kuweka ngome mashariki mwa taifa hilo.
Vikosi mbalimbali vya wapiganaji nchini humo vimegawanyika kutokana na msimamo mpya wa utawala na baada ya umoja wa mataifa kuingilia kati harakati za kuliunganisha taifa.
|
0 Comments