Waziri mkuu wa Iceland, Sigmundur Gunnlaugsson amejiuzuru kufuatia kashfa nyaraka za siri huko Panama zinazohusiana na ukwepaji wa kodi. Gunnlaugsson imebainika kuwa anamiliki kampuni ya Wintris yeye na mke wake na kwamba hakuweka wazi umiliki huo baada ya kuingia katika bunge la nchi hiyo
Waziri huyo mkuu Iceland awali alikuwa akituhumiwa kuficha mamilion ya dola na mali zinazomilikiwa na familia yake.
Sigmundur anasema kuwa alihamishia hisa za kampuni hiyo kwa mke wake na amepinga kuhusika na jambo lolote baya.Hata hivyo baadhi ya raia walioandamana nje ya bunge la nchi hiyo wamesema kuwa hatua ya kujiuzuru pekee yake haitoshi kwa kiongozi huyo kutokana na kashfa hiyo
Mmoja wa raia walioandamana katika nje ya jingo la bunge amesema kuwa yupo hapo kwasababu bado anaona serikali haijajiuzuru kutokana na kashfa hii,kwa sababu Waziri wa Fedha na Waziri wa Mambo ya ndani bado wapo madarakani, wamegoma kujiuzuru wakati wote wana akaunti hizo za kashafa”
Rais Barack Obama akizungumzia kashafa hiyo pia amesema kuwa jitihada zinatakiwa ilikuweza kuziba mianya yote ukwepaji kodi.Hata hivyo kuwa idara za fedha za Marekani zimekwisha chukua hatua kukabiliana na mianya hiyo ya kukwepa kodi.
|
0 Comments