Shirika la madaktari wasio na mipaka limesema robo tatu ya watu wazima wenye maambukizi ya virusi vya Ukimwi Magharibi na Afrika ya kati wapo katika mazingira yasiyowaruhusu kupata Matibabu.
Pamoja na idadi hiyo kubwa ya watu wazima wasio katika mazingira rafiki kwa matibabu,shirika hilo la Medecins Sans Frontieres linasema asilimia 90 pia ya watoto wadogo wenye maambukizi ya virusi hivyo vya Ukimwi wanakabiliana na vikwazo kupata huduma za kiafya

MSFlimesisitiza kuwa kama hakutakuwa na jitihada za makusudi kuhakikisha huduma za afya kwa waathirika hao zinafika Afrika Magharibi na kati na vinginevyo,malengo kutokomeza maambukizi ya ugonjwa huo ifikapo 2020 hayatafanikiwa.
Ripoti hiyo imeleza kuwa takribani watu milioni tano katika ukanda wa Afrika hawapati dawa za kupunguza makali ya virusi vya ugonjwa wa Ukimwi,ambapo zaidi ya asilimia 20 ya watu wana maambukizi ya virusi katika eneo hilo,huku nusu tu ndiyo wanaoweza kufikiwa na matibabu.
Hata hivyo takwimu za shirika hilo zinaonyesha kuwa idadi ya watu wenye maambukizi ya virusi vya ukimwi Afrika Magharibi na kati ni ndogo ikilinganishwa nchi za kusini mwa Afrika ambapo nusu ya idadi ya watu wote wanamaabukizi na nusu yao pia wapo katika mazingira mazuri kupatiwa matibabu.