1
Kikosi cha Uokoaji kikiopoa mwili wa mmoja wa watu waliokuwa kwenye gari hilo.
WATU wawili wanasadikiwa kufariki dunia baada ya gari aina ya Toyota Hiace walilokuwemo kuserereka wakati likiingia katika kivuko na kutumbukia baharini leo eneo la Kivukoni jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa taarifa za awali kutoka kwa mkuu wa kikosi cha Uokoaji cha Zimamoto, tayari mwili wa mtu mmoja mwanaume umepatikana na jitihada za kusaka mwili wa mtu mwingine anayesadikika kuwa ni mwanamke zinaendelea.
2
Zoezi la uokoaji likiendelea.
Mashuhuda wa ajali hiyo wanaeleza kuwa chanzo cha gari hiyo kuingia na kuzama baharini kimetokana na kile kinachodaiwa kufeli kwa breki wakati dereva wa gari hiyo akikata kona kuelekea upande wa mbele ambapo gari zenye uharaka zinapewa nafasi kukaa mbele pindi kivuko kitakapofika ziwe za kwanza kuingia katika kivuko hicho.
3
Kikosi cha Zimamoto na Uokoaji kikiwa eneo la tukio.
Kaka ambaye ni manusura wa ajali hiyo anasema, ndugu hao waliotumbukia kwenye gari akiwemo dada yake ambaye bado jitihada za kumtafuta zinaendelea kwa pamoja walikuwa wakitokea mkoani Mbeya kwenye msiba.