Mazungumzo ya amani kuhusu mzozo wa kisiasa Burundi, ambayo yalipangiwa kufanyika wiki ijayo mjini Arusha, yameahirishwa.
Mashauriano hayo yalikuwa yamepangiwa kufanyika kuanzia tarehe 2 hadi 6 Meichini ya mfanikishi aliyeteuliwa na Jumuiya ya Afrika Mashariki, Rais wa zamani wa Tanzania Benjamin Mkapa.
Taarifa kutoka afisi ya Bw Mkapa imesema mazungumzo hayo yameahirishwa kutoa nafasi kwa mashauriano zaidi na wadau.
“Inakadiriwa kwamba mazungumzo haya yatafanyika katika wiki ya tatu ya mwezi Mei,” taarifa hiyo imesema.
Awali, Bw Mkapa alikuwa ameeleza matumaini kwamba pande zote zingeshiriki.
Lakini siku chache baadaye upande wa serikali nchini Burundi ulilalamika kwamba haukuwa umepokea mwaliko rasmi.
Siku moja baadaye, serikali hiyo ilidokeza kwamba ingeshiriki.
Tulifikaje hapa?
|
0 Comments