Kituo kikiwa kimeng’olewa kutokana na ujenzi wa kituo cha kuuzia mafuta, GBP.
Stori: Issa Mnally na Makongoro Oging’, UWAZI
Mkurugenzi wa Kampuni ya GBP inayosafirisha na kuuza mafuta ndani na nje ya nchi anadaiwa kupuuza,kudharau na kutotii agizo la serikali la kumtaka kusitisha mara moja ujenzi wa kituo cha mafuta kilichopo Keko Magurumbasi, Wilaya ya Temeke Mkoa wa Dar es Salaam, hali iliyotafsiriwa na wakazi wa eneo hilo kuwa anachezea ‘masharubu’ ya Mkuu wa Mkoa wa Dar, Paul Makonda.

Gazeti hili limefanikiwa kupata nakala ya barua aliyoandikiwa na Afisa Mtendaji wa Kata ya Keko, Dominic Kassongo ya Machi 4,mwaka huu yenye kumbukumbu namba TMC/KKW/UJ/04/16 ikimtaka Mkurugenzi wa GBP kusimamisha mara moja ujenzi katika viwanja namba 63/1/2 na 42 kitalu 9 Keko.
Sehemu ya barua hiyo imesema: “Ukaguzi uliofanyika katika eneo hilo imegundulika kuwa unafanya ujenzi tofauti na kibali ulichopewa cha kufanya matengenezo ya kituo cha mafuta, aidha umefanya ujenzi nje ya eneo la kiwanja chako na kufikia Barabara ya Chang’ombe,kitendo ambacho kimesababisha uharibifu wa barabara na kutishia uhai wake.”
….Ujenzi ukiendelea.
Ikaendelea: “Kwa mapungufu haya nakuamuru kusitisha mara moja ujenzi unaoendelea,kubomoa ukuta uliojenga barabarani na urejeshe jengo ndani ya mipaka ya kiwanja chako. Amri hii itekelezwe ndani ya siku tatu kuanzia tarehe ya barua hii na kukaidi kutaniongoza kukuchukulia hatua kali za kisheria.”
Mtendaji huyo akizungumza na gazeti hili ofisini kwake wiki iliyopita, alisema kwamba mkurugenzi huyo hajatii amri hiyo.
Mtendaji huyo akizungumza na gazeti hili ofisini kwake wiki iliyopita, alisema kwamba mkurugenzi huyo hajatii amri hiyo.
“Niliamua kuchukua hatua ya kumwandikia barua baada ya wananchi kulalamika kwa Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Keko Magurumbasi na alipomuambia aache kuvamia kituo cha mabasi na eneo la barabara, akapuuzwa, nimeshatoa taarifa wilayani lakini hakuna kilichofanyika,” alisema mtendani huyo.
Wananchi wa eneo hilo kwa nyakati tofauti walisema kuwa kitendo cha mfanyabiashara huyo kuidharau serikali ni aibu kubwa huku wakimuomba Mkuu wa Mkoa wa Dar, Makonda kuingilia kati.
RC Makonda.
“Tunamuomba RC Makonda aingilie tatizo hilo kabla halijakomaa, huyu bwana amebomoa kibanda cha stendi cha kujikinga jua na mvua na amekificha ndani ya uzio wake, amekuwa akisababisha ajali za mara kwa mara kutokana na ufinyu wa barabara, daladala zinashusha na kupakia barabarani,” alilalamika Ally Issa, mkazi wa Keko Magurumbasi.
Februari 29 na Machi 17, mwaka huu, waandishi wa habari hii walikwenda makao makuu ya kampuni hiyo yaliyopo Kurasini, walipouona uongozi ulisema upelekewe maswali kwa maandishi, ambapo Machi 23 ulipelekewa ukaahidi kutoa majibu Machi 31, hata hivyo walipofuatwa wakasema hawajashughulikia suala hilo.
0 Comments