1
Mkazi wa Toraja, Sulawesi Kusini, nchini Indonesia akiwavisha nguo ndugu zake waliokufa siku za nyuma.
UNAWEZA usiamini! Huko Toraja, Sulawesi Kusini, nchini Indonesia, wakazi wa huko wana mila ambayo kuna wakati wanawafukua ndugu zao waliokufa – wakiwemo watoto wadogo – wakawaosha, wakawafanyia kila usafi na
kuwavisha nguo mpya za kuvutia.
2
Kwa mujibu wa wakazi wa eneo hilo ambao husema wafu hao huendelea kuishi katika mioyo na akili zao, wanadai marehemu hao huendelea kutembea maeneo mbalimbali duniani wakiwa kama misukule au mizimu.
8
Wakati wa utaratibu huo ambao unajulikana kama Ma’nene, maiti hao hubebwa kutoka sehemu walizofia au kuzikwa na baada ya kufanyiwa mchakato huo wa kijadi, hutembezwa maeneo mbalimbali ya Jimbo la Sulawesi wakiwa katika mstari mmoja.
7
Baada ya utamaduni huo, maiti hao hurejeshwa katika majeneza ambayo hukarabatiwa ikiwa yameharibika wakati wa kuwatoa maiti au majeneza mapya hununuliwa kwa ajili ya kuwahifadhi tena.
5
Utaratibu huo wa Ma’nene ambao humaanisha ‘Sherehe ya Kuwasafisha Maiti’, hufanywa na watu wa Toraja kwa imani ya kuzirudisha roho za wafu katika vijiji vyao.
4
Hivyo, iwapo mtu alifariki akiwa safarini, familia huwajibika kwenda mahali alikofia na kumsindikiza kurejea nyumbani kwa kumtembeza hadi kijijini.
3
Katika siku za nyuma, watu wa eneo hilo walikuwa wanaogopa kusafiri mbali, wakiogopa kwamba pindi wakifia huko wasingeweza kurejea vijijini kwao.
6