Bodi ya kutathmini na kutoa msamaha kwa wafungwa nchini Israel imekataa kumwachilia huru rais wa zamani wa nchi hiyo Moshe Katzav.
Katzav ametumikia miaka minne ya kifungo chake cha miaka saba jela alichohukumiwa baada ya kupatikana na makosa ya ubakaji.

Kupitia taarifa, bodi hiyo imesema Bw Katzav ameendelea kujitazama kama mwathiriwa na kulalamika kuhusu gharama kubwa ambayo familia yake imelipia.
Bodi hiyo imesema hajaonekana kujutia kitendo chake wala kuonyesha huruma kwa wanawake aliowashambulia.
Bw Katzav alihudumu kama rais wa Israel kuanzia 2000 hadi 2007.