Raia wa Uingereza walio na mizizi yao nchini Somalia wanakutana mjini Bristol mashariki mwa Uingereza kujadiliana kuhusu kuwazuia watu wa jamii hiyo kuwekwa itikadi kali.
Waandalizi wanasema kuwa vijana wengi wa Kisomali kutoka Uingereza wamejiunga na makundi ya itikadi kali nchini Syria,Iraq na Somalia kwenyewe.
Kundi la wapiganaji wa kisomalia al-Shabab huwaonyesha wapiganaji wake raia wa Kisomali katika hatua yake ya propaganda.
Mkutano huo unawakutanisha wawakilishi wa jamii,makundi ya kidini wanaharakati na maafisa wa polisi