Follow us: Subscribe via RSS Feed Connect on YouTube Connect on YouTube
Maganga One Blog kwa habari za kitaifa,kimataifa,burudani na michezo kila siku. Tutumie habari na matukio yoyote kwa email yetu ya magangaone@gmail.com

May 19, 2016

Aliyeingia ndani ya kasri la Malkia akamatwa

Mwanamme mmoja amekamatwa ndani ya makao ya kifalme nchini Uingereza ya Buckingham baada ya kuvuka ua.
Mwanamme huyo wa umri wa miaka 41 alipatikana katika uwanja wa kasri hilo dakika saba baada ya ving'ora kuanza kulia siku ya Jumatano jioni.

Mshukiwa huyo ambaye hakuwa na silaha yoyote alikamatwa kwa kushukiwa kuingia eneo linalolindwa na sasa yuko kizuizini.
Image captionMalkia Elizabeth
Inafahamika kuwa Malkia alikuwa ndani ya kasri wakati wa kisa hicho.
Kumeshuhudiwa utata mara kadha kwenye ulinzi wa kasri la Buckingham miaka ya nyuma, kikiwemo kisa cha Michael Fagan ambaye aliingia hadi chumba cha kulala cha Malkia mwaka 1982, na kukaa kwa muda wa dakika 10 akizungumza na malkia kabla ya Malkia kufanikiwa kupiga king'ora wakati mtu huyo alipoomba sigara.

Share this article :

0 Maoni:

 
Maganga One Blog © Copyright 2017. All Rights Reserved.

Powered by Maganga One.
Back to TOP