Follow us: Subscribe via RSS Feed Connect on YouTube Connect on YouTube
Maganga One Blog kwa habari za kitaifa,kimataifa,burudani na michezo kila siku. Tutumie habari na matukio yoyote kwa email yetu ya magangaone@gmail.com

May 25, 2016

Bill Cosby atakiwa mahakani

Jaji nchini Marekani ameamuaru mchekeshaji, Bill Cosby, kusimama mahakamani dhidi ya kesi kwa madai ya unyanyasaji wa kijinsia.
Cosby anatuhumiwa kwa makosa ya kumdhalilisha wanawake katika makazi yake mnamo mwaka 2004 baada ya kumlewesha kwa kitu kinachodaiwa dawa za kulevya.

Mchekeshaji huyo,ambaye awali kabla ya masahibu haya alikuwa ni mmoja miongoni mwa wachekeshaji maarufu wa runinga nchini Marekani, tayari amekwisha kumbana na misukosuko ya kukabiliwa na wimbi la madai unyanyasaji wa kijinsia.
Wanawake waliowengi, ambao alikuwa na mahusiano nao miaka ya 1960 wao hawawezi tena kufungua mashtaka ya jinai.Kufuatia hali hiyo Cosby amekana madai yote yanayomkabili.
Mwezi uliopita mahakama ya rufaa ilitupilia mbali madai yanayomkabili Cosby na kusema kwamba alikuwa kinga ya mashtaka kutoka upande wa mashitaka na aliyekuwa Mwanasheria wa wilaya muongo mmoja uliopita.

Share this article :

0 Maoni:

 
Maganga One Blog © Copyright 2017. All Rights Reserved.

Powered by Maganga One.
Back to TOP