Follow us: Subscribe via RSS Feed Connect on YouTube Connect on YouTube
Maganga One Blog kwa habari za kitaifa,kimataifa,burudani na michezo kila siku. Tutumie habari na matukio yoyote kwa email yetu ya magangaone@gmail.com

May 25, 2016

ELIZAYO HB KUTOKA JIJINI MWANZA AIRUDIA NGOMA YA RAYMOND-KWETU KWA USTADI WA HALI YA JUU.

Kwetu ni Wimbo unaofanya vizuri nchini na hata nje ya nchini ambapo kwa mara ya kwanza uliimbwa na Msanii Raymond kutoka WCB Wasafi. 


Kutokana na wimbo huo kuwa na mashairi mazuri pamoja na melodi yenye kuvutia, Msanii Elizayo HB kutoka Jijini Mwanza ameurudia wimbo huo na kuuongezea ladha ambayo inaufanya kuwa wimbo bora uliorudiwa kwa sasa nchini.


"Nimeamua kuurudia wimbo huu kwa sababu umebeba ujumbe mzito ambao ulinigusa na kuamua kuurudia kwa njia zangu za pekee ili watanzania wayasikie maneno vizuri pasipo na shaka". Elizayo HB ameiambia BMG.

Hakika Elizayo HB ameutendea haki wimbo huo ambayo umerekodiwa katika Studio za Brother's Music Jijini Mwanza, kwa ushirikiano wa producers Adof pamoja na Doncha Master.
Bonyeza HAPA Kusikiliza Au Play Hapo Chini.
Share this article :

0 Maoni:

 
Maganga One Blog © Copyright 2017. All Rights Reserved.

Powered by Maganga One.
Back to TOP