Jiji la London limemchagua Meya wa kwanza Muislamu, Sadiq Khan, aliyekuwa wakati mmoja Waziri katika chama cha upinzani cha Laba.
Bwana Khan ni mwana wa dereva wa zamani wa bas jijini London aliyezaliwa Pakistan. Alipata kura milioni moja na mia tatu elfu.

Hicho ni kiwango kikubwa sana cha kura kuwahi kupigiwa Meya ye yote jijini London.
Image copyrightPA
Image captionSadiq Khan akishirikiana na wakaazi wa jiji la London
Katika hotuba yake ya ushindi, Bwana Khan aliahidi kuongoza kwa niaba ya wakaazi wote wa London.
Wasimamizi wa kampeni ya mpinzani wake katika uchaguzi huo Zac Goldsmith, ambaye ni tajiri mkubwa walishutumiwa kwa kudai kuwa Bwana Khan ana uhusiano na Waislamu wenye itikadi kali.
Bwana Khan alisema kuwa wakaazi wa London wamepiga kura ya umoja na kuponza mgawanyiko.
Image copyrightGetty
Image captionMeya mpya wa jiji la London Sadiq Khan
Ushindi huo ni wa kumtia moyo kiongozi wa chama cha Labour Jeremy Corbyn.
Chama chake kilipata ushindi dhaifu katika maeneo mengine ya nchi katika uchaguzi huo.