Image copyright
Image caption

Wakuu wa Jamhuri ya Demokrasi ya Congo wanasema wamemkamata naibu kamanda wa kundi la wapiganaji, linalohusishwa na mauaji makubwa ya Rwanda ya mwaka 1994.
Msemaji wa serikali, alieleza kuwa Jenerali Leopold Mujyambere, wa kundi la Rwanda la FDLR, alikamatwa mjini Goma, mashariki mwa nchi.



Image copyrightGetty
Image captionFDLR kisangani

Kundi la FDLR ni la Wahutu wanaoshutumiwa kuuwa malaki ya Watutsi na Wahutu waliokuwa na msimamo wa wastani, wakati wa mauaji ya kimbari ya Rwanda.
Rwanda imeingilia kati kijeshi mashariki mwa Congo katika juhudi za kuliangamiza kundi hilo.