Klabu ya soka ya Leicester City wameshinda taji la ligi kuu England katika historia inayovutia kwenye ligi hiyo. Suluhu ya 2-2 waliyoipata Tottenham dhidi ya Chelsea siku ya jumatatu usiku ilisababisha mafanikio hayo makubwa kuwahi kutokea kwa upande wa Claudio Ranieri.
Image copyrightAP
Image captionMashabiki wa timu ya Leicester City
Leicester walianza kampeni zao za ubingwa huku wakipewa nafasi moja tu kati ya 5000 kushinda taji la ligi na pia wakitoka katika janga la kutaka kushuka daraja.

Lakini wamepoteza michezo mitatu tu katika kile kinachotafsiriwa kama hadithi za kale na ushindi wa kipekee katika timu hiyo. Wapinzani wao wa karibu Spurs,Arsenal,Manchester City, Manchester United na washindi wa ligi msimu uliopita Chelsea wameshindwa kuwazuia mbweha katika msimu mzima wa ligi.
''Kwa kigezo cha soka la ndani,Leicester City kushinda taji la ligi kuu ni mafanikio makubwa sana katika historia na haiwezi kusahaulika'' kiungo wa zamani wa Leicester Robbie Savage ameiambia BBC.''Ni jambo la ajabu.Hii ni hatua ya mageuzi katika historia ya Ligi Kuu."
Rais wa shirikisho la soka duniani Gianni Infantino amesema historia nzuri ya Leicester ilikua ni kama hadithi za kale.