Na Mwandishi wetu, Dar es Salaam


MUZIKI wa kizazi kipya
maarufu kama ‘Bongo Flava’ ulikuwa
haujulikani na pia haukuonekana kama ni sanaa halisi ya muziki;  hivi ndivyo ambavyo vizazi vilivyotanguliwa vlivyoutazama
takribani miongo miwili iliyopita japo ni muziki wa kuburudisha watu wa rika zote
wadogo kwa wakubwa.

Muziki wa ‘Bongo Flava’ umebadilisha himaya ya
muziki hapa Tanzania ambao umepata sifa  katika nchi za Afrika mashariki, Afrika na
Ulaya.

Ni ukweli usiofichika
kuwa, sekta ya muziki wa kizazi kipya imekuwa kwa kasi na hata kuwapatia ajira
vijana wengi wa kitanzania wenye vipaji ambao walikuwa hawana kazi hapa nchini
kufuatia tatizo la ajira ambalo limekuwa ni changamoto kwa vijana.

Ingawaje fani ya muziki
imwekuwa ikionekana kuwa na maendeleo yanayosuasua kwa kipindi cha muongo mmoja
hivi, wasanii wa muziki bado wanakumbana na changamoto nyingi.

Wameeleza changamoto
hizo kuwa ni mapungufu ya kuwezeshwa kitaifa na kimataifa na kuwepo kwa ujuzi
mdogo miongoni mwa wanamuziki.

Kuna baadhi ya
makampuni, mashirika na hata watu binafsi ambao wameona umuhimu wa kutatua
matatizo kama haya yanayowakabili wasanii na wanamuziki hapa nchini, na badala
yake wamegundua mikakati ya kuwawezesha ili kutimiza malengo na ndoto zao kwa
ujumla.

Tigo Tanzania ni moja
ya makampuni hayo, na kwa kuwa ni kampuni ya kidijitali inayobadili maisha ya
watumiaji mtandao wake, kampuni hii ilianzisha jukwaa la wanamuziki wa kizazi
kipya ijilikanayo kama ‘Tigo Music Platform’ 
ambayo inalengo la kuwawezesha wasanii wa muziki hapa nchini na kufanya
kazi zao zijulikane ndani na nje ya nchi.

Hadi sasa Tigo
imekwisha wawezesha wanamuziki wa kitanzania wapatao 20 kupitia program yake ya
Tigo Music Platform tangu ilipoanzishwa mnamo mwezi Januari 2015.

Wakiongea katika nyakati tofauti, baadhi ya wanamuziki ambao
wamefaidika na  program ya Tigo Music walisema
kuwa kupitia jukwaa hilo, miziki ya watanzania na wasanii wa muziki
wamejulikana kimataifa.

Hii ni kwa sababu kuwa washabiki wa muziki hasa wa kizazi
kipya kutoka kila kona hapa duniani wamekuwa wakipata miziki hii kupitia mfumo
wa kusambaza miziki hiyo kwa njia ya mtandao wa kimataifa ujulikanao kama
‘streaming’.

“Kwa kupitia mtandao huu, wasanii wa muziki wa kitanzania
wamepata fursa ya kujulikana kimataifa, na vile vile kuweza kupata fedha za ziada
kutokana na mmiziki yao, na hii ndiyo ilikuwa lengo kuu la kuanzisha mtandao
huu unaowaunganisha na washabiki wa miziki hiyo”, alisema mawanamuziki nguli wa
Bongo Flava mwenye asili ya Kongo, Christian Bella katika mahojiaono maalumu
mwaka jana. 

Taarifa kutoka Tigo inasema kuwa, program ya Tigo Music pia
inatoa mafunzo kwa wanamuziki ili kuwajengea uwezo wasanii wa muziki hasa wa
kizazi kipya wanaoibukia ili wajue ualisia wa mali zao kama muziki kuwa ni mali
na masoko pia ili waongeze ujuzi wao na kujenga maisha yao kuwa bora.

“Mtandao wa kusambaza miziki duniani kote unakuwa kwa haraka,
na vilevile ni wa pili kujilikana kama mtandao wa simu kusini mwa bara la
Afrika”, inasema taarifa hiyo na kuongeza kuwa huu ni mtandao wa kidijitali kwa
ajili ya maisha ya kisasa ambao Tigo imeutumia kuwezesha ukuaji wa vipaji vya
wasanii wa muziki wa kizazi kipya.

Inaendelea kusema kuwa Tigo imekuwa ikiwatia moyo wanamuziki
wa ndani kuwa karibu na shirika la haki za muziki barani Afrika, yaani ‘Africa
Music Rights’ ambao huwadhamini na kupandisha chati haki za muziki barani
Afrika ili wanamuziki waweze kutawala soko la muziki hapa Afrika.

Kwa sasa Tigo Tanzania imekuwa karibu sana na kampuni ya
kimataifa ya kifaransa ambayo kazi yake kubwa ni kusambaza miziki duniani
ijulikanayo kama ‘Music Streamer Deezer’.

Kampuni hii hutoa huduma zake kwa ajili ya kusambaza na
kupata miziki zaidi kote duniani kupitia simu za mkononi, ambapo inatoa njia 36
milioni za kutapa miziki mbalimbali duniani.

 Akizungumzia mtandao
wa muziki wa Tigo yaani ‘Tigo Music’ wakati akihojiwa jijini Dar es Salaam,
mwanamuziki wa kizazi kipya wa muziki wa ‘Bongo Flava’ ambaye ni mmoja wa
wanaofaidika na mtandao huu, David Genz maarufu kama ‘Yangdee’ alisema kuwa
program ya muziki wa Tigo Music imemuwezesha kujulikana katika nyanja ya
kitaifa na kimataifa.

Yangdee aliongeza na kusema: “kuanzishwa kwa program ya ‘Tigo
Music Platform’ ni ukombozi kwa wanamuziki wachanga wanauibukia hapa nchini kwa
kuwa imetuwezesha kujulikana kimataifa, tunaishuukuru kampuni ya Tigo Tanzania
kwa kutusaidia”.

Alikuwa akiongea wakati alipokuwa na wenzake ambao pia wanaonufaika
na mpango huu wa Tigo Music wakati walipotembelea moja ya maduka ya Tigo
yaliyopo jijini Dar es Salaam katika ziara maalumu iliyolenga kubadilishana
mawazo kuhusu kazi zao za muziki.

 Christian Bella naye
anaongeza kuwa anaishukuru Tigo kwa ubunifu wake hasa pale ilipoanzisha program
hii ya Tigo Music ya kuwawezesha wanamuziki wa kitanzania.

 Katika mahojiano yake
na waandishi wa habari yaliyofanyika katika ofisi za Tigo makao makuu, Bella
alisema: “ninayo heshima kubwa kuisifu Tigo kwa kuwa imepandisha chati miziki
ya wasanii hapa Tanzania”. Ni matumaini yangu kuwa msaada wa Tigo utaendelea
kuwasaidia wanamuziki wa Tanzania katika kukuza fani ya muziki nchini”.

Tigo Music ilizinduliwa hapa Tanzania mwezi Januari 2015
ambapo Meneja wa Nembo wa Tigo, Bw. William Mpinga alisema kuwa ina lengo la
kukuza kazi za wanamuziki na kuendeleza ukuaji wa soko la wanamuziki wa ndani.



MWISHO