Meli ya kifahari ya Marekani imeanza safari yake kuelekea Cuba ikitokea nchini Marekani kwa mara ya kwanza katika kipindi cha zaidi ya miaka hamsini iliyopita.
Meli hiyo iitwayo Adonia, imebeba abiria wapatao mia saba,imeng'oa nanga kutoka katika bandari ya Miami na inatarajiwa kufika tamati ya safari yake Jumatatu ijayo.

Cuba na Marekani zimerejesha uhusiano baina yao wa kidplomasia mwaka wa jana, ingawaje vita baridi iliyokuwa baina ya nchi hizo ilisababisha hali kibiashara kati yao kuwa ya kusua sua na bado hali si shwari mpaka sasa.
Image copyrightAFP
Safari hiyo ya kihostoria kwa njia ya maji imepiga hatua moja kubwa mbele katika kuuimarisha uhusiano huo wa kidlomasia na hii ni baada ya serikari ya Cuba kukubali kuondoa marufuku ya raia wake kuingia nchini Marekani ama kutumia maji kama njia ya usafiri kuingia nchini humo.