Follow us: Subscribe via RSS Feed Connect on YouTube Connect on YouTube
Maganga One Blog kwa habari za kitaifa,kimataifa,burudani na michezo kila siku. Tutumie habari na matukio yoyote kwa email yetu ya magangaone@gmail.com

May 21, 2016

MSAADA KWA MTOTO AHMED

Waungwana popote duniani mlipo tunaomba kwa unyenyekevu mkubwa kwa yoyote atayeguswa amsaidie mtoto Ahmed{2yrs}.
Ahmed amezaliwa akiwa na miezi 9,ni mtoto mwenye matatizo ya ugonjwa unaoitwa {CELEBRAL PALSYS}.Ugonjwa huo husababishwa na uharibifu wa ubongo na kumsababisha mtoto kushindwa kufanya harakati zozote za kimwili,kama kula,kulia na hata kucheka.Ahmed amekuwa kitandani toka kuzaliwa kwake mpaka hivi sasa.Kwa rehema za Allah matibabu ya maradhi yake yamepatikana nchini Malaysia kwa asilimia 90 mtoto Ahmed kupona.

Maombi kwa kila mwenye moyo wa kujitolea mkusaidia matibabu ya mtoto Ahmed.Jumla ya gharama zote za matibabu ya mtoto ni dola za Kimarekani 45,000.Msaada wako unaweza kusaidia kupona kwa mtoto Ahmed.
Kwa wakazi wote waliopo nchini Tanzania utaratibu wa kumtumia pesa mtoto huyo ni kama ufuatavyo.
Simu namba 0677 999 567{ Mama wa Mtoto}
TIGO PESA 0657384444
MPESA 0753964451

Akaunti ya Benki namba 066 2135158 BARCLAYS BANK

Na kwa  wakazi waliopo nje ya nchi Tutumie Bank ya nchini Nederland ijulikanayo kwa jina la ING BANK
Kupitia Account No. NL75 ING B 008217577 kwa jina la T Ahmed Ali.

Ndugu muungwana popote ulipo mchango wako kiasi chochote kile utakachojaaliwa tunakuomba ili umsaidie mtoto huyu.Tunakuomba pia uusambaze ujumbe huu kadri uwezavyo.
Mungu atakulipa kwa wema wako.


 

Share this article :

0 Maoni:

 
Maganga One Blog © Copyright 2017. All Rights Reserved.

Powered by Maganga One.
Back to TOP