Rais wa Uganda Yoweri Museveni,amempandisha cheo mwanaye na kufikia ngazi ya Meja Jenerali.
Muhoozi Kainerugaba anatambulika kama mtu mwenye nguvu sana katika jeshi la nchi hiyo na wengi wanaamini kuwa anatengenezwa kwa ajili ya kumrithi baba yake ambaye amekuwa madarakani kwa miaka 30 sasa.

Jenerali Kainerugaba amepinga kuwa baba yake anajitengenezea siasa za kifalme, laikini pia akiweka wazi malengo yake ya kuwa mwanasiasa.
Museven alipata ridhaa ya kuiongoza Uganda kwa kipindi cha miaka 5 mwezi Februari kufuatia uchaguzi mkuu ambao pia ulishutumiwa vikali na jumuiya ya ulaya na Marekani.