Kiongozi wa zamani wa upelelezi nchini Uingereza amesema operesheni kubwa zaidi zinahitajika maeneo ya mwambao wa Afrika ya Kaskazini kwa lengo la kuondoa mgogoro wa wahamiaji haramu wanaoingia Ulaya.
Richard Dearlove ambaye alikuwa kiongozi katika shirika la Uingereza la Upelelezi amesema kuwa operesheni hizo zinaweza kuanza mara moja uwapo mazingira ya kisiasa nchini Libya yataruhusu Umoja wa ulaya kufanya kazi zake katika eneo hilo.

Katika mazungumzo yake na BBC amesema kuwa mchakato unaoendeshwa na umoja wa ulaya katika kukabiliana na suala hilo kuwa upo taratibu sana na sio wa uhakika,huku akitoa onyo la ongereko la watu Ulaya kama watashindwa kuzuia wahamiaji hao.
Pia amekosoa mpango wa EU wa kutoa hati ya usafiri (visa) bure kwa raia wa Uturuki wa kuingia na kutoka Uturuki bure na kuacha wahamiaji kwenda Ugiriki.