Yoweri Museveni leo atatawazwa rasmi kuwa Rais mpya wa Uganda kwa muhula wa saba mfululizo.
Tayari Rais Museveni amekwisha tawala miaka 30. Kutawazwa kwake leo, ambako kutashuhudiwa na viongozi wa mataifa 14 kutoka Afrika na wageni wengine mashuhuri, kuna fuata ushindi uliojaa ubishani katika uchaguzi wa Februari 18.

Na leo rasmi imetangazwa kuwa siku ya mapumziko ili watu watokeze kwa wingi kwa sherehe hizo. Ingawaje bado kuna hali ya wasiwasi kwa vile chama cha upinzani na FDC na mgombea urais wa zamani Dk Kizza Besigye bado wanakana ushindi wa Museveni.
Museveni kumkabidhi madaraka Museveni si jipya kwa Waganda. nani Rais ambaye alilaumu mwaka 1986, viongozi wa Afrika kukaa madarakani kwa muda mrefu sana.
Wasiwasi upo, kutokana na hatua kali za usalama zinazochukuliwa. Usiku utawaona askari polisi na jeshi wakipiga kwata mitaa mhumu mjini Kampala.
Mitandao ya kijamii kama Facebook na Twiter imezimwa. Pia, serikali ikitegemea amri ya Mahakama ya Katiba kupiga marufuku malalamiko ya ukinzani na kuwekwa hewani na vyombo vya habari, jana, Dk Kizza Besigye, anayebisha ushindi wa Museveni kwa dhati, alikamatwa tena baada ya kusemekana kuapishwa kama rais mafichoni.
Mashirika ya haki za binadamu na uhuru wa kujieleza, ndani na nje ya Uganda, yameikosoa serikali kwa hatua za kigandamizi. Lakini Waziri Mkuu, Ruhakana Rugunda, amejibisha kwa kuyashtumu kuugua mayopia, kutoona mbali: