Kuanzia mwaka ujao wa 2017, Serikali ya Indonesia itapiga marufuku raia wake kwenda hadi katika mataifa ya kigeni, ili kufanya kazi za nyumbani.
Lakini bado wataruhusiwa kwa kiasi fulani kufanya kazi za uyaya ikiwa tu wataishi eneo tofauti na waajiri wao, kufanya kazi kwa saa kadhaa na kuhakikishiwa kuwa wataruhusiwa kupata siku za mapumziko.

Maafisa wakuu nchini Indonesia, wamepitisha mapendekezo hayo ya muda mrefu yenye nia ya kuwalinda wafanyikazi na sasa itatangazwa rasmi hivi karibuni kama ilivyopangwa.
Maelfu ya raia wa Indonesia kwa sasa wanafanya kazi za nyumbani katika mataifa ya kigeni hasa mashariki mwa Asia na mashariki ya kati huku wengi wao wakiishi na waajiri wao.